MAAZIMIO YA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA 2018-TANZANIA

Kuelekea kilele cha siku ya kimataifa ya Vijana, Umoja wa mataifa Tanzania,Pathfinder kwa kushirikiana UNFPA,DSW na Wadau mbalimbali wa maendeleo ya Vijana waliandaa mdahalo Maalumu uliohusisha Vijana wasiopungua 250 katika Ukumbi wa Mikutano Afrika Mashariki mjini Jijini Arusha, vikihusisha wawakilishi wa vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kama vile Asasi za kiraia, Ofisi ya wazirim kuuki tengo cha Vijana, wawakilishi kutoka wizarambalimbali ikiwemo ile ya Vijana, Wadau wa Maendeleo, wajasiriamali, Walemavu,Wanazuoni, Vyombo vya habari na Sekta mbalimbali zikiwemo zile za binafsi pamoja na mitandao ya Vijana kutoka katika kada mbalimbali,ambapo.Katika Mdahalo ule Vijana walipata nafasi ya kuchangia mawazo yao kwa kutambua na kuya jua Mazingira salama Kwa maendeleo yao vijana na jamii kwa ujumla                                        IMG-20180813-WA0039

Siku hii pia iliambatana na kauli mbiu ya maadhimisho haya ambayo ni :Mazingira salama kwa vijana .Kauli mbiu hii ya siku ya Vijana duniani inahusisha lengo nambari 8,11 na 13 kutoka kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu,Kabla ya hapo vijana pia walishiriki zoezi la kupandamiti 500 kwa kushirikiana na wananchi wa wilaya ya Arumeru wakishirikiana kwa karibu na mkuu wa wilaya Mh.Jerry Muro,na pamoja na wananchi wa wilaya hii ilikukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa wa arusha ,Lakini tuliweza kutembelea maeneo mbalimbali na kuona kazi mbalimbali za zinazofanywa na vijana kama vile ujasiria mali na wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya vijana kutoka kata ya King’ori,Ndili youth center pamoja na makundi mengine kwenye wilaya ya Hai na Arusha Mjini,Zoezi hili lilisimamiwa na Timu ya vijana wenyewe,wadau wa maendeleo pamoja na PSW Tanzania.Pamoja na Hayo,Baadhi ya vijana Walipata Mafunzo maalumu ya malengo ya maendeleo endelevu kutoka kwa jamii zote za umoja wa mataifa Tanzania.

IMG-20180814-WA0182

Katika kutengeneza mazingira salama kwa vijana,Tumeona mchango mkubwa sana unaofanywa na Serikali na Wadau mbali mbali katika kuleta fursa za kijamii,kiuchumi,kisiana,kielimu na hata kwenye maeneo ya burudani na michezo

Bonyeza Hapa kupata Maazimio ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2018 MAAZIMIO-YA-SIKU-YA-KIMATAIFA-YA-VIJANA-YALIOFIKIWA-NA-VIJANA- (22 downloads)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *